Kocha Mkuu wa Simba,
Zdravko Logarusic amesema mchezo wao wa kirafiki keshokutwa Jumamosi, utakuwa
sehemu nzuri ya kukipanga kikosi vizuri kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.
Logarusic raia wa
Croatia amesema anatarajia mechi hiyo itakuwa ni nzuri na tofauti na zile za
michuano ya Mapinduzi hasa katika suala la kupanga timu.
“Kweli tulikuwa
tunapanga timu kwa ajili ya mashindano na kujiandaa na ligi, lakini michuano ni
michuano tu.
“Mechi ya Mtibwa
imekuja wakati mwafaka na ikiwezekanba tunaweza kuomba moja kwa ajili ya
kujiimarisha zaidi.
“Kuna mambo lazima
tutarekebisha, lakini kuna mambo tumejifunza kwenye michuano ya Mapinduzi
ambayo tutayafanyia kazi.
“Kawaida katika mchezo
wa soka mnajifunza kila siku na hata katika ufundidishaji lazima urudie zaidi
ya mara moja ili kitu kiwangie vizuri wachezaji na waweze kukikumbuka wakati wa
utekelezaji,” alisema.
Katika mechi ya mwisho
Simba ililala bao 1-0 dhidi ya KCC ya Uganda katika fainali ya Kombe la
Mapinduzi.
Mara ya mwisho Simba
kucheza Uwanja wa Taifa jijini Dar, iliilaza Yanga kwa mabao 3-1 katika mechi
ya Nani Mtani Jembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment