Uongozi wa Yanga umewataka wanachama wa klabu
hiyo kujitokeza kwa wingi kwneye mkutano utakaofanyika Jumapili Januari 19
kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga,
amesema leo, mkutano huo utafanyika kuanzia Saa 3:00 asubuhi.
Sanga amewataka wanachama kujitokeza kwa wingi
kwa kuwa hiyo ndiyo nafasi nzuri kwao kutoa na kufikisha mawazo yao kwa lengo
la kusaidia ujenzi wa maendeleo klabu hiyo.
Makamu huyo mwenyeki, alisema ndani ya mkutano
huo watajadili mambo kadhaa muhimu yanayohusiana
na klabu yao ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati madhubuti ya kutetea ubingwa.
Pamoja na hivyo, kwa pamoja wanachama hao
watapanga mikakati imara ya kujiandaa na mashindano yenye malipo ya juu zaidi
kwa ngazi ya klabu ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, hasa kama timu itafanikiwa
kusonga mbele zaidi.
Awali Sanga alikuwa amezungumzia uamuzi wao
wa kumpa Kocha, Hans van Der Pluijm, vyeo vitatu vya mkurugenzi wa ufundi, kocha
mkuu na meneja.
Tayari kocha huyo raia wa Uholanzi yuko
nchini Uturuki ambako ameungana na kikosi cha Yanga kilichoweka kambi nje
kidogo ya mji wa Antalya.
0 COMMENTS:
Post a Comment