Pamoja na
kurejea kikosini, kiungo nyota Athumani Iddi ‘Chuji’ hatacheza katika mechi ya
Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komoronize ya Comoro.
Chuji alipata
kadi ya nyekundu katika mechi dhidi ya Zamalek ya Misri wakati Yanga ikishiriki Ligi
ya Mabingwa Afrika, mwaka juzi.
Chuji ambaye
amerejea Yanga baada ya kusimamishwa muda usiojulikana tayari yuko kambini
Bagamoyo.
Habari za Chuji kukosa mechi hiyo zimethibitishwa na msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto.
Alijiunga na
kikosi hicho na tayari kocha Hans van Der Pluijm ameonyesha kuikubali kazi yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment