Na Saleh
Ally
KOCHA wa
Arsenal, Arsene Wenger si mtu mwenye mambo mengi, vituko au mbwembwe na hana
rekodi ya kuwa na wachezaji wenye vituko.
Taarifa za
kwamba anavutiwa na uwezo wa mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Mario
Balotelli zimeonyesha kuwashitua wengi, lakini yeye ameendelea kuwa kimya.
Wenger
amekuwa kimya lakini tayari taarifa zimevuja kwamba wadhamini wao wapya wa
vifaa, Kampuni ya Puma ya Ujerumani, wameahidi kufanya kila linalowezekana
kuhakikisha mtukutu huyo anatua Emirates.
Uongozi wa
Arsenal umekaa kimya kuhusiana na suala hilo la juhudi za kumtoa Balotelli
kutoka AC Milan na kumrejesha England akipige katika klabu yao ya Arsenal.
Hiyo ni
dalili kuwa kweli Wenger anamhitaji Balotelli kwa ajili ya kuimarisha kikosi
cha kwanza msimu ujao, iwe ametwaa ubingwa au la.
Hawezi
kuwa mjinga kwa kujishusha kwa Balotelli, muhimu kwake ni mafanikio, ndiyo
maana Alex Ferguson aliwahi kusafiri hadi Ufaransa kumbembeleza Eric Cantona
aliyekuwa amevuruga na baadaye kurejea kwao kwa kiburi.
Kawaida
makampuni yote yanayodhamini, hupenda kuona sehemu wanayoingiza fedha zao
kunakuwa na mafanikio makubwa ili kuwatangaza wao zaidi.
Kwa kuwa
Arsenal wameonyesha wanamhitaji Balotelli, Puma wanaamini kama atajiunga na
Arsenal, macho na masikio kwa wingi zaidi yataelekezwa kwa timu hiyo na
kuwasaidia wao kujitangaza zaidi.
Lakini taarifa
nyingine zinaeleza hizo zilikuwa juhudi za Puma kutaka kumshawishi Balotelli
kuingia upande wao na kuachana na Nike mara tu mkataba wake ulipomalizika,
ambapo tayari amejiunga na Puma.
Puma
wamefanikiwa kuing’oa Nike katika kikosi cha Arsenal baada ya kutoa mkataba
mnono zaidi ikiwa ni katika kampeni zao za kurudi kwenye chati ya juu hasa
katika soka.
Utukutu:
Inaonekana
Wenger hana rekodi ya kuwa na wachezaji watukutu kama ilivyo kwa Balotelli
ambaye ana tabia za kupigana hadi na wenzake mazoezini.
Wakati
fulani, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Man City, Roberto Mancini, alilazimika kumkwida
kwa kuwa alionekana si muelewa.
Kazi
ambayo Wenger hawezi kuifanya hata iwe vipi na swali ni kama Balotelli atakuwa
amebadilika maana tangu alipoondoka England, tayari katika umri wake mwaka
mmoja umeongezeka.
Tafrani:
Achana na
kuwa mgomvi, vituko vingine vya Balotelli ni kuonekana kwenye klabu za usiku
hata siku moja kabla ya mechi.
Ukali wa
Mancini kiasi fulani ulichangia kupunguza, wataalamu wa masuala ya soka nchini
England, wanasema Wenger ni kati ya makocha wakali huenda kuliko wote na hataki
mchezo.
Kama ni
hivyo, basi haitakuwa kazi ngumu kukabiliana na tafrani hizo za Balotelli
ambaye anajulikana kwa kipaji na utukutu.
Kiwango:
Kiwango
chake kimeporomoka, hizi ni hisia za wengi lakini kwa ufuatiliaji mzuri na
majibu ya takwimu zake zinaonyesha bado moto wake ni uleule.
Huenda
ndiyo maana Wenger ‘amenusa’ kama ilivyo kawaida yake na kuamua kuweka kando
utukutu wake na kuangalia kazi yake.
Msimu wa
2011-12 alicheza mechi 40, hapa ni zile za Ligi Kuu England alizochezea kikosi
chake cha Man City. Kati ya hizo 25 alianza na 15 kuingia na alifanikiwa
kufunga mabao 19.
Msimu
wa 2012-13 alicheza mechi 45, kati ya
hizo 31 alianza na 14 aliingia na hadi mwisho pamoja na timu ya taifa,
alifanikiwa kufunga mabao 23.
Pamoja na
kuuanza vizuri msimu huu, wakati unakwenda ukingoni mambo yanaonekana si shwari
sana kwake. Maana amecheza jumla ya mechi 31, kati ya hizo sita akiwa ameingia
na tayari ana mabao 18.
Yote
yanawezekana, kikubwa hapa ni kusubiri kipindi cha usajili kikianza, halafu
tutaona.
Takwimu za msimu huu kwa klabu:
MECHI 16
MABAO 9
PASI ZA MABAO 3
MASHUTI 99
Fin.
0 COMMENTS:
Post a Comment