Baadhi ya wanaodaiwa kuwa
ni viongozi wa Azam TV, juzi walizua varangati baada ya kutokea mvutano kati
yao na vyombo vingine vya habari vilivyokuwa vikirekodi katika video mechi ya
Ligi Kuu Bara kati ya Mtibwa Sugar na Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Awali wapiga picha mbalimbali
waliweka mitambo yao sawa na kuanza kurekodi baadhi ya matukio kabla ya mechi
hiyo, lakini baada ya muda wahusika wa Azam TV waliwavaa na kuwaamuru waache
kurekodi.
Alipofuatwa mmoja wa mabosi wa Azam TV ambaye hakutaja jina lake, alisema walisahau kutoa
taarifa mapema juu ya taratibu zilizopo sasa kwa kuwa wao ndiyo wenye mamlaka
ya kurekodi michezo hiyo katika video.
“Hawakujua taratibu zetu,
ila tumebahatika kuwazuia, anayetaka matukio muhimu lazima afuate taratibu,
hatuna kipingamizi cha kuwapatia,” alisema.
Azam TV ndiyo yenye mkataba
na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wa kurekodi na kuonyesha mechi za ligi
hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment