Klabu ya Yanga imetangaza rasmi vituo kumi
vitakavyouza tiketi la pambano lao la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Komorozine
ya Visiswa vya Comoro itakayopigwa Jumamosi ya wiki hii kwenye uwanja wa Tiafa
jijini Dar.
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kiziguto amesema
wamechapa tiketi 45,000 kwa ajili ya
mashabiki wake na wataanza kuziuza keshokutwa Ijumaa kupitia vituo vya:
Sokoni Kariakoo, Oil Com- Buguruni, Dar Live,
Uwanja wa Uhuru, Steeaz Samora, Oil Com Ubungo, Kimara mwisho, Mwenge stendi,
Shule ya Benjamini Mkapa na basi maalum ambalo litakuwepo klabuni.
Viingilio vitakuwa kama ifuatavyo: VIP A 30,000
( tiketi 500), VIP B&C 20,000 (4500), Orange 10,000 (7000) na viti vya Bluu
na kijani 5000 (33,000).
Aidha alisema wapinzani wao wanatarajia kuwasili
leo Jumatano kupitia shirika la ndege la Air Tanzania na kesho watafanya
mazoezi kwenye uwanja wa Karume na Ijumaa watahamia uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment