Uongozi wa klabu ya Yanga ni kama umeonyesha
hofu ya kumtumia au kutomtumia mshambuliaji Emanuel Okwi kwenye mechi ya
Jumamosi dhidi ya Wacomoro kwa kuwa mpaka sasa hawajapata taarifa kutoka TFF
kama wanaweza kumtumia.
Awali Okwi alizuiwa na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) wakidai mpaka wajiridhishe Fifa kama Yanga wanapaswa kumtumia
mchezaji huyo aliyejiunga akitokea Sports Club Villa ya Uganda.
Ofisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema
mchezaji huyo licha ya kuwa amepitishwa na Shirikisho la Soka la Afrika Caf
lakini wao wanasubiri tamko kutoka TFF ambao nao wanasubiri majibu kutoka Fifa.
“Tunachosubiri ni kupewa ‘go a head’ kutoka TFF,
lakini mchezaji wetu amepitishwa na Caf kuichezea Yanga kwenye michuano hiyo
kwa kuwa tulimsajili kwa kufuata kanuni zote na ITC tukapata,” alisema Kizuguto
na kuongeza:
“Tumepewa taarifa na Caf kutukumbusha tusimtumie
kiungo wetu Chuji kwa kuwa katika mchezo wa mwisho alipata kadi nyekundu dhidi
ya Zamalek.”
0 COMMENTS:
Post a Comment