Bayern Munich imetoa tena ubingwa wa
Bundesliga baada ya kuicgapa Hertha Berlin kwa mabao 3-1.
Licha ya kuwa ugenini, Bayern imetwaa
ubingwa huo huku ikionyesha kiwango cha juu kama ambavyo ilitarajiwa na wengi.
Kocha Pep Guardiola ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona, naye ameweka rekodi
ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya kwanza na msimu wa kwanza akiwa
kocha wa timu.
Mabao ya Bayern katika mechi hiyo
yalifungwa na Toni Kroos katika dakika ya 6, Mario Goetze dakika ya 14 na Frank
Ribery akamalizia kazi katika dakika ya 79 wakati lile la kufutia machozi
lilifungwa na Adrian Ramos kwa penalty katika dakika ya 66.
Bayern imetwaa ubingwa huo huku ikiwa na
mechi saba mkononi, hali inayoonyesha kuwa ukali wake msimu huu ilimaliza kabisa
ushindani wa Ujerumani.
0 COMMENTS:
Post a Comment