Manchester City imezidi kuongeza kasi ya
kuukimbilia ubingwa, lakini ikaongeza kujenga heshima baada ya kuwachapa watani
wao Manchester United kwa mabao 3-0.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England
iliyomalizika punde, Eden Dzeko alifunga mabao yote mawili ya City.
Bao la kwanza katika dakika ya kwanza tu
baada ya mabeki wa United kuzubaa naye akamalizia kiulainiii.
Pamoja na kujitutuma, Dzeko alifunga bao
la pili katika dakika ya 56 baada ya Fellaini na Rio Ferdinand kujichanganya
wakati wa kuokoa.
Yaya Toure aliyeng'ara naye akapiga bao la tatu kwa shuti kali la kimo cha panya.
SWANSEA VS ARSENAL (2-2)
Swansea wakiwa nyumbani walionyesha wamepania kufanya kweli baada ya kufunga bao katika dakika ya 11.
Lakini Arsenal wakaamka na kusawazisha katika dakika dakika ya 73 kabla ya Olivier Giroud kutupia la pili katika dakika ya 74.
Lakini dakika ya 90, kiungo Flamini alijifunga hivyo kufanya matokeo yawe sare ya 2-2.
NEWCASTLER VS EVERTON (0-3)
Everton nayo ikaendelea kuchanja mbuga,
licha ya kuwa ugenini ikashinda kwa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wake Newcastle.
Wafungaji ni Ross Barkley katika dakika
ya 22 na Romelu Lukaku katika dakika ya 52.
Leon Osman naye akafunga bao la tatu zikia zimebaki dakika mbili tu kabla ya mpira kwisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment