Kipa namba moja wa Yanga, Deogratius
Munish ‘Dida’ ameumia mkononi ingawa haijajulikana sababu ni nini.
Dida ameweka picha kwenye mtandao wa
kijamii wa Facebook inayoonyesha jeraha ambalo limepatiwa matibabu na kusema
kuwa ameumia.
PICHA ALIYOWEKA |
Kutokana na hali hiyo, wakati Yanga
ikiivaa Mtibwa Sugar leo, kipa Juma Kaseja alishika nafasi hiyo ya Dida huku
benchi akikaa Ally Mustapha ‘Barthez’ ambaye sasa ni kipa namba tatu.
Dida
ndiye amekuwa kipa chaguo la kwanza tokea Kocha Hans van Pluijm alipotua nchini
na kuanza kuinoa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment