Kocha Jose Mourinho amesema ameshangazwa na kauli ya Yaya Toure ambayo inaonyesha ni mtovu wa nidhamu dhidi yake.
Mara baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa, Man City ikiwa imetolewa na Barcelona, Toure alisema hivi: “Mourinho amekuwa akizungumzia kila timu, kila mtu, inatakiwa awe na nidhamu kiasi fulani. Ndiyo maana wakati yuko hapa (Hispania), Madrid ilikuwa inafungwa kila inapokutana na Barcelona.”
Baada ya kauli hiyo, Mourinho kama kawa, alijibu: “Inanishangaza sana kwa tabia hiyo ambayo si ya kawaida, inaonyesha Toure ni mtovu wa nidhamu. Mimi nilisema tokea awali kuwa Arsenal na City wana vikosi bora.
“Wanaweza kubadili mambo wakiwa ugenini na hawapaswi kudharauliwa, sasa nashangaa anayosema yanatokea wapi. Au anataka nisiseme lolote.
“Mfano leo nasema United ni bora kuliko Olympiakos, sasa nitashangaa nikisikia na Rooney, Van Persie, Carrick au Ferdinand wakisema Mourinho hana nidhamu!”
0 COMMENTS:
Post a Comment