Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) linavikumbusha vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuwa vinatakiwa
kuwasilisha majina ya mabingwa wao kufikia Machi 30 mwaka huu.
Majina ya mabingwa yanatakiwa
kuwasilishwa pamoja na usajili wa wachezaji waliotumika kwenye ligi ya mkoa.
Kila klabu inaruhusiwa kuongeza wachezaji watano kutoka ndani ya mkoa husika,
ambapo unatakiwa uthibitisho wa usajili huo.
Mpaka sasa ni vyama viwili tu ndivyo
vimeshawasilisha mabingwa wao. Vyama hivyo ni Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Pwani (COREFA) ambapo bingwa wake ni Kiluvya United, na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Lindi (LIREFA) ambapo bingwa ni Kariakoo SC.
0 COMMENTS:
Post a Comment