Mshambuliaji
wa Yanga, Emmanuel Okwi amesema anataka kufunga lakini mambo hayakai sawa.
Jambo hilo
limekuwa likimpa wakati mgumu na amepania kupata mabao katika mechi zinazofuata
za Yanga.
Akizunguma
na SALEHJEMBE, Okwi amesema ingawa anatakiwa kutengeneza nafasi za mabao kama
ambavyo amekuwa akifanya, lakini anatamani kufunga.
“Zaidi ya
mechi mbili sasa, sijisikii vibaya lakini nataka kufunga mabao na kuisaidia
timu yangu.
“Ninajua
nina uwezo huo, lakini mambo huwa yanakataa wakati fulani.
“Mechi
zijazo tutashirikiana zaidi na ninaamini ninaweza nikafunga au kutengeneza
nafasi zaidi,” alisema.
Mganda
huyo amekuwa akitengeneza nafasi nyingi zaidi za mabao katika kikosi cha Yanga,
lakini Yanga imekuwa na tatizo la kupoteza nafasi hizo za kufunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment