Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig
amesema anamkumbusha mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage kuhusiana na fedha
zake.
Ingawa hajasema kiasi gani kilichobaki
lakini katika ujumbe wake kupitia mtandao wa kijamii, Liewig amesema anahitaji
fedha zake.
“Najaribu kumtafuta mwenyekiti (Rage),
lakini imekuwa kimya na kawaida hapokei simu. Mwambie ninahitaji fedha zangu zilizobaki.
“Yeye anajua ni kiasi gani, mwambie
ninaishi vijijini na siwezi kuwa kwenye mtandao kila wakati kuwasiliana naye,”
alisema.
Simba ilimlipa baadhi ya fedha zake za
mshahara na kuvunja mkataba wake wakati ilipomtupia virago Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment