MWOMBEKI AKIPAMBANA |
Kocha Mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko
Logarusic, amefunguka na kuainisha sababu zinazomfanya asimchezeshe na
kumjumuisha kikosini mshambuliaji wake Betram Mwombeki.
Loga alisema kwamba huwa anashindwa
kumtumia mchezaji huyo si kwa sababu nyingine binafsi wanazohisi watu ila kila
anapotaka kumtumia humkuta hayupo fiti kutokana na kuwa majeruhi mara kwa mara
na hivyo huamua kumweka pembeni na kuwatumia wengine.
“Suala lipo hivi, nashindwa kumchezesha
Mwombeki kwa sababu hayupo fiti, haiwezekani kila mara mchezaji anakuwa
majeruhi halafu bado nimwamini kwa asilimia zote na kuendelea kumpa nafasi
kwenye mechi.
“Anapokuwa majeruhi na kukosekana
mazoezini nashindwa kumuona kama yupo fiti kiasi gani kwa ajili ya mchezo
unaokuja pia anaelewana na wenzake kwa kiasi gani, hii inanisaidia mimi kujua
nimpange acheze na nani na kwa mfumo upi.
“Sasa Mwombeki kila baada ya mechi moja
au kila baada ya mazoezi ya siku mbili au tatu anaumia, mtu kama huyo pia
anakosa pumzi kwenye mechi kwa kuwa hana
maandalizi ya kutosha.
“Hali hii inanifanya nimpange mchezaji
mwenye uhakika wa kucheza dakika 90 kuliko yeye ambaye atacheza kwa dakika 20
au 25 na ni lazima awe mchezaji wa dakika hizo kwa kuwa ana mazoezi hafifu,”
alisema Loga na kuongeza:
“Sidhani kama atapata nafasi kwenye
kikosi changu,” alisema Loga.
0 COMMENTS:
Post a Comment