Kocha Mkuu wa
Simba, Zdravko Logarusic amesema mechi ya leo dhidi ya Coastal Union ni kama
vile mtihani wa mwisho kwa mwanafunzi.
Logarusic
ameiambia SALEHJEMBE kwamba anaamini kama watapotea katika mechi dhidi ya
Coastal Union, basi nafasi mbili za ubingwa na ile ya pili zinaweza kuwa ngumu
kwao.
“Lazima
kushinda Jumapili (leo) dhidi ya Coastal, kama tutapoteza basi tutakuwa
tumejiondoa kabisa kwenye ubingwa na kuchukua nafasi ya pili.
“Mechi
itakuwa ngumu lakini tuna kila sababu ya kushinda kwa kuwa tuna kikosi kizuri
na chenye uwezo,” alisema Logarusic.
Simba iko
katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 36 nyuma ya Azam FC, Yanga na Mbeya City
ambazo zinazidi kuchanja mbuga.
0 COMMENTS:
Post a Comment