KIKOSI CHA SIMBA |
Simba
haitakuwa katika mbio za kuwania ubingwa, lakini unaweza kusema hata nafasi ya
pili pia ni nadra.
Kwani leo
imepoteza mchezo wake dhidi ya Coastal Union baada ya kufungwa kwa bao 1-0
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
BOCCO KAZINI |
Wakati
Simba wakilazwa na Coastal Union iliyojaa vijana, Azam FC wamezidi kujichimbia
kileleni baada ya kuifunga JKT Oljoro kwa bao 1-0.
John Bocco ‘Adebayor’
ndiye aliyefunga bao hilo muhimu kwa Azam FC ambayo sasa imefikisha pointi 47,
mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa
Azam Complex jijini Dar.
Simba
wanabaki na pointi 36 baada ya kupoteza mchezo huo wa Coastal Union licha ya
kuwa nyumbani.
Nafasi wanayoweza
kuijutia ni ile katika dakika ya 90 aliyoipata Ramadhani Singano ‘Messi’ akiwa
amebaki na kipa wa Coastal lakini kashindwa kuusukuma mpira wavuni.
Kupitia Chanongo,
Amissi Tambwe na Jonas Mkude, Simba ilipoteza nafasi zaidi ya sita za wazi za
kufunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment