Mbeya City imeendeleza ubabe kwenye Ligi Kuu Bara baada ya
kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Katika mechi hiyo ngumu kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi
jijini Dar es Salaam, Mbeya City ilipata bao kila kipindi.
Mfungaji alikuwa mmoja tu, Saad Kipanga aliyefunga la kwanza
katika dakika ya 10 na la pili katika dakika 69.
0 COMMENTS:
Post a Comment