Kocha Mkuu we
JKT Ruvu, Fred Felix Minziro amesema pamoja na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa
Mbeya City, jana, bado wana nafasi ya kupambana na kubaki Ligi Kuu Bara.
Minziro
ameiambia SALEHJEMBE kwamba kikosi chake bado kina nafasi ya kufanya vizuri na
kubaki katika ligi hiyo lakini lazima wajitume.
“Unajua
kwenye mpira ukifanya makosa, halafu ukakutana na mtu makini basi ni lazima
akuadhibu.
“Mabeki
wetu hawakuwa makini ndiyo maana sasa tunajutia lakini pointi tatu dhidi ya
Mbeya City zilikuwa muhimu sana.
“Lakini
nina imani tutajirekebisha mechi zijazo na kufanya vizuri, tukijituma na kuwa
makini, bado tuna nafasi,” alisema inziro.
0 COMMENTS:
Post a Comment