Mambo yako hivi, mshambuliaji wa Simba raia wa Burundi, Amissi Tambwe, ni bora zaidi ya
yule wa Yanga, Emmanuel Okwi, ambaye alijiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea
kwenye kikosi cha Villa ya Uganda.
Ubora huo
wa Tambwe unatokana na mchezaji huyo kumfunika vibaya Okwi ndani dakika 540
ambazo kila mmoja amezitumia uwanjani hivi karibuni akiitumikia klabu yake
kwenye michuano ya ligi kuu na ile ya kimataifa ambayo Yanga ilishiriki.
Tangu mwezi
huu uanze Tambwe ameitumikia Simba dhidi ya Mgambo JKT, Prisons, Ruvu Shooting,
JKT Ruvu, Mbeya City na Coastal Union, wakati Okwi aliongoza Yanga dhidi ya
Ruvu Shooting, Al Ahly, Mtibwa Sugar, Azam na Rhino Rangers.
Championi
Jumatano limebaini hilo baada ya kuwafuatilia wachezaji hao katika mechi hizo
sita ambazo wamezitumikia klabu zao hizo ndani ya mwezi huu.
Katika
uchunguzi huo, ilibainika kuwa Tambwe ndiye aliyefanya vizuri zaidi ya Okwi
kwani ndani ya dakika hizo 540 alizoitumikia Simba katika mechi hizo za ligi
kuu amefanikiwa kufunga mabao manne.
Kwa upande
wake Okwi yeye amezifumania nyavu mara moja katika dakika hizo 540
alizoitumikia Yanga mpaka sasa tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea SC
Villa ya Uganda.
Tambwe
alifunga mabao hayo katika mechi za ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu, Ruvu Shooting
na Mbeya City wakati Okwi bao lake hilo alilifunga katika mchezo wa ligi kuu
dhidi ya Ruvu Shooting.
Hata hivyo,
Okwi alipoulizwa kuwa ni kwa nini ametumia muda mwingi uwanjani huku akiwa
amezifumania nyavu mara moja alisema: “Wachezaji
wengi wananikamia sana hivyo inanibidi nichukue jukumu la kuwatengenezea nafasi
za kufunga wachezaji wanzangu na siyo kwamba nimeshuka kiuchezaji, kiwango
changu kipo juu ila wananikamia sana,” alisema Tambwe.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment