BOUZIANI AKIZUNGUMZA JAMBO WAKATI WA UTAMBULISHO WA SMART MBELE YA WAANDISHI WA HABARI. |
Mtandao
mpya wa simu wa Smart umepanga kuwajali wanamichezo mbalimbali nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa Smart, Abdellatif Bouziani, amesema watashirikiana na
wanamichezo mbalimbali kadiri siku zitakavyokuwa zinasonga mbele.
Akizungumza
na gazeti hili jijini Dar es Salaam, Bouziani alisema mtandao wao utafanya
mambo kadhaa ya kijamii na mojawapo ni michezo.
“Kwa sasa
tuko katika nchi tatu za Afrika Mashariki, Uganda, Burundi na sasa Tanzania.
Tunajua namna michezo inavyopendwa.
“Hivyo
tutafanya chini juu kuhakikishia ushirikiano wetu na wanamichezo unakua,”
alisema.
Kuhusiana
na ushindani, Bouziani alisema ubora wa
mtandao na unafuu ndiyo utakaowavutia wengi.
“Lakini
huduma zetu ni nzuri, usione tumeingia sasa Tanzania ukadhani ni wageni katika
huduma za simu. Tuko sehemu mbalimbali duniani hivyo tuna uzoefu na ushindani
tunauweza,” alisema akionyesha kujiamini.
0 COMMENTS:
Post a Comment