Simba
imetangaza rasmi kuwa uchaguzi wake mkuu utafanyika Mei 4, mwaka huu.
Tarehe
hiyo ya uchaguzi imetangazwa rasmi mara tu baada ya kikao cha kamati ya
utendaji ya klabu hiyo kukutana.
Akizungumza
leo jijini Dar, Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Asha Muhaji amesema Mwanasheria
maarufu nchini, Dokta Damas Daniel Ndumbaro ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kati
hiyo ya uchaguzi.
Makamu
wake anakuwa, Salum Madenge na Katibu ni Issa Batenga na msaidizi wake ni Khalid
Kamguna.
Muhaji
aliwataja wajumbe kuwa ni katibu mkuu wa zamani wa Simba, Kassim Dewji, Juma
Simba na katibu mkuu wa zamani wa DRFA, Amin Bakhresa.
Kuhusiana na mkutano wake wa kesho, Muhaji alisisitiza Simba itafanya mkutano huo kwa ajenda ileile, moja ya marekebisho katiba.
0 COMMENTS:
Post a Comment