Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
inaendelea kesho (Machi 19 mwaka huu) kwa mechi kati ya Yanga na Azam
itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo
zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika magari maalumu kwenye vituo vya Shule ya
Sekondari Benjamin Mkapa, Ubungo Terminal, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa
Samora/Ohio, OilCom Ubungo, Buguruni Shell, Dar Live- Mbagala, kituo cha
daladala Mwenge na Uwanja wa Taifa.
Baada ya saa 6 mchana mauzo yote
yatahamia Uwanja wa Taifa ambapo milango kwa ajili ya mechi itakuwa wazi
kuanzia saa 7.30 mchana.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa
sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati viti vya rangi ya
chungwa, bluu na kijani kiingilio ni sh. 7,000.
Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi
Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ambapo atasaidiwa na Anold Bugado (Singida),
Florentina Zablon (Dodoma) na Lulu Mushi (Dar es Salaam). Kamishna wa mechi
hiyo Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza
wa Mwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment