Wachezaji 31 wameteuliwa kujiunga na
timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa
ajili ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini
Senegal.
Ngorongoro Heroes itakayokuwa chini
ya Kaimu Kocha John Simkoko akisaidiwa na Mohamed Ayoub inaingia kambini kesho
(Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kwanza dhidi
ya Kenya itakayochezwa kati ya Aprili 4-6 jijini Nairobi.
Kikosi kinachounda timu hiyo ambayo
itarudiana na Kenya kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Dar es Salaam
kinajumuisha pia baadhi ya wachezaji walioonekana katika mpango wa ung’amuzi wa
vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi
Manula (Azam), Hamad Juma Hamad (Scouting- Temeke), Manyika Peter Manyika
(Scouting- Ilala) na Mwinyi Hassan Hamisi (Mtende, Zanzibar).
Mabeki wa pembeni ni Ayoub Semtawa
(Coastal Union), Edward Charles (JKT Ruvu), Frank Linus Makungu (Scouting-
Rukwa), Gabriel Gadiel Michael (Azam), Hussein Mkongo (Ashanti United) na
Ibrahim Said Mohamed (Chuoni, Zanzibar). Mabeki wa kati ni Bashiru Ismail
(Tanzania Prisons), Faki Rashid Hakika (Ashanti United) na Pato Ngonyani
(Majimaji).
Viungo ni Ally Nassoro (Coastal
Union), Bryson Raphael (Azam), Farid Musa (Azam), Hamid Mohamed (Mbeya City),
Hassan Mbande (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mohamed Ibrahim (Scouting- Ilala), Idd
Seleman (Ashanti United), Mohamed Issa Juma (Acudu, Afrika Kusini), Muhsin Ally
Muhsin (Scouting- Kinondoni), Seleman Magoma (Scouting- Ruvuma) na Tumaini John
(Scouting- Mwanza).
Washambuliaji ni Ally Salum Kabunda
(Ashanti United), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto, Zanzibar), Jafari Mwambusi
(Mbeya City), Kelvin Friday (Azam), Ramadhan Bilal (Mlale JKT), Salum Abdilah
Mineli (Ndanda) na Sibiank Lambard (Tanzania Prisons).
0 COMMENTS:
Post a Comment