YAHAYA |
Katika hali isiyo ya kawaida inayotokana
na mgogoro wa kifedha uliopo ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), huenda
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikavunjwa.
Bodi ya Ligi iko chini ya Yahya Mohammed
ambaye ndiye mwenyekiti wa kwanza aliyeshinda uchaguzi.
Chanzo cha ndani kutoka bodi hiyo kilisema
kuwa kwa sasa hali siyo shwari kabisa na muda wowote kuna uwezekano wa bodi
hiyo kuvunjwa kutokana na kuwa na mgororo wa masuala ya kifedha uliopo baina
yake na shirikisho, kitu ambacho kinaendelea kwa sasa na si kizuri.
Chanzo hicho kilisema kuwa kutokana na
mgawo mdogo ambao wanaupata TFF, pande hizo mbili zimeshindwa kuelewana na
kupelekea kuwepo kwa dalili za uwezekano wa kuvunjwa kwa bodi hiyo.
“Ni kweli hapo Bodi ya Ligi kwa sasa kuna
mgogoro kati yake na Shirikisho la Soka Tanzania na tatizo kubwa ni masuala ya
fedha ndiyo yanayotukwamisha hasa kwenye mgawanyo na huenda bodi ikavunjwa muda
wowote na kutokuwepo tena,” kilisema chanzo.
Championi lilimtafuta Rais wa TFF, Jamal
Malinzi, kuzungumzia suala hilo na alisema kuwa hana taarifa ya namna hiyo.
“Sina taarifa ya namna hiyo na ndiyo
kwanza nakusikia wewe unazungumzia suala hilo, ladda kama kuna jambo jingine,”
alisema kisha akakata simu.
0 COMMENTS:
Post a Comment