Mshambuliaji nyota wa Azam FC, Kipre
Tchetche, raia wa Ivory Coast, ametuma salamu kwa wachezaji wa Yanga kwa
kuwaambia kuwa watapata kazi ngumu ya kumzuia leo.
Yanga inavaana na Azam kwenye mchezo wa
Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Timu hizo zilipokutana kwenye mzunguko
wa kwanza, Azam iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, hivyo mchezo huu unaonekana
kuwa mkali kwa pande zote.
Kipre amesema anajua wazi kuwa mchezo
huo utakuwa mkali lakini yeye na wachezaji wenzake watahakikisha wanatoka na
pointi zote tatu ili kuzidi kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu Bara.
Alisema hawaidharau Yanga lakini kwa
kuwa yeye yupo Azam kwa ajili ya kuhakikisha wanafanya vizuri, basi ni wazi
kuwa japo atapata upinzani mkubwa kutoka kwa mabeki wa Yanga, lazima ashinde
kwa kuwa hiyo ndiyo kazi yake iliyompeleka katika timu hiyo.
“Najua Yanga ni timu nzuri, itatupa upinzani
mkubwa, lakini mimi nimekuja hapa Azam kwa ajili ya kufunga mabao na
kuhakikisha timu inapata ushindi katika kila mechi, basi pia nitafanya hivyo
katika mchezo na Yanga,” alisema Tchetche.
0 COMMENTS:
Post a Comment