Kocha Mkuu wa Kenya, Adel Amrouche
ametua nchini akiongozana na Mkurugenzi wa Ufundi wa Kenya, Jacob ‘Ghost’ Mulee
ili kuipa nguvu timu yao ya vijana.
Amrouche raia wa Ubelgiji amesema kikosi
chao cha timu ya taifa ya vijana kina nafasi leo dhidi ya wenyeji Tanzania,
Ngorongoro.
Timu hizo za Tanzania na Kenya chini ya
miaka 20, leo kwenye Uwanja wa Taifa jijibni Dar zitacheza mechi yao ya pili
kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana. Katika mechi ya kwanza
mjini Machakos, Kenya, timu hizo zilitoka sare ya bila bao.
Akizungumza mara baada ya kuwasili
jijini Dar es Salaam, Amrouche alisema wanaheshimu uwezo wa Tanzania, ila
wanachotaka kufuzu.
“Najua kocha wa timu yetu anajua la
kufanya, tuko hapa kumuunga mkono na kusaidia ushauri ni kipi cha kufanya. Niko
na Mulee hapa na tunaamini Kenya itafuzu,” alisema kocha huyo bora wa Ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati.
Amrouche ambaye amefikia kwenye hoteli
ya Sapphire pamoja na kikosi hicho ambacho kipo nchini siku tatu zilizopita,
awali alikuwa Kocha Mkuu wa Burundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment