Mario Balotelli haishi vituko, kwani jana usiku alisimama ghafla
na kuanza kumlaumu kocha wake, Clarence Seedorf kwa kumtoa.
Katika mechi hiyo, AC Milan ikiwa ugenini iliendelea kupoteza
mechi za Serie A baada ya kufungwa na wenyeji wake AS Roma huku Miralem Pjanic
na mchezaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho wakitupia bao mojamoja na
kutengeneza ushindi wa mabao 2-0.
kitendo cha kutolewa nje katika kipindi cha pili kilimuudhi Balotelli ambaye alianza kumlaumu Seedorf ambaye alionekana kuwa mtulivu akimuangalia.
0 COMMENTS:
Post a Comment