Kifo cha kocha wa zamani wa Barcelona, Tito Vilanova, kimewaunganisha
wachezaji wa karibu timu zote za Hispania na duniani kote kumuombea na kuipa
pole familia yake.
Wachezaji wa Real Madrid, Atletico Madrid na timu nyingi za
England, Italia wamekuwa wakituma salama za pole kwa uongozi wa Barcelona
pamoja familia ya marehemu.
Vilanova amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 45,
ugonjwa wa kansa ndiyo chanzo cha kifo chake na ulianza kumuandama kuanzia
mwaka 2011.
Msimu uliopita, alilazimika kuacha kazi yake ya ukocha wa Barcelona baada ya
hali yake kutokuwa nzuri na akapelekwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu.
Kabla ya kuwa kocha mkuu wa Barcelona, Vilanova alikuwa
msaidizi wa Pep Guardiola na kikosi chao kilifanya vizuri sana.
0 COMMENTS:
Post a Comment