AMROUCHE, MULEE WAKIJADILI JAMBO KWENYE GAZETI LA CHAMPIONI WAKIWA NA KIKOSI CHA CHAMPIONI BAADA YA KUTEMBELEA OFISI ZA GAZETI HILO, LEO. |
Makocha wawili mahiri katika ukanda wa
Afrika Mashariki leo walitembelea katika ofisi za gazeti la namba moja la
michezo na burudani la Championi jijini Dar es Salaam.
AMROUCHE AKIONYESHWA KAZI YA CHAMPIONI NA MHARIRI WA CHAMPIONI IJUMAA, JOHN JOSEPH |
AMROUCHE AKIJADILI JAMBO NA SALEH ALLY. KUSHOTO NI MHARIRI WA CHAMPIONI JUMATANO, PHILLIP NKINI. |
Kocha wa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee
Stars’ na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Jacob ‘Ghost’
Mulee walitembelea katika ofisi za Championi na kupokelewa na Mhariri wake
kiongozi, Saleh Ally ‘Jembe’.
Wakiwa ofisini hapo, Mulee na Amrouche
ambaye ni Kocha Bora wa Afrika Mashariki na Kati kwa kipindi hiki walipata
nafasi ya kuonyeshwa magazeti ya Championi yanavyoandaliwa na utaratibu wake.
SHIGONGO )KULIA) AKIWAKARIBISHA GHOST MULEE NA AMROUCHE OFISINI KWAKE (WA PILI KULIA NI MHARIRI KIONGOZI WA CHAMPIONI, SALEH ALLY) |
Pia waliweza kuzungumza na viongozi
mbalimbali wa Kampuni ya Global Publishers, akiwemo Mkurugenzi wake, Eric James
Shigongo ambaye alibadilishana nao mawazo kuhusiana na mambo mbalimbali ya
kimichezo.
Akizungumzia ugeni huo, Saleh Ally,
alisema Ghost amekuwa kama ndugu yake tokea alipofahamiana naye kwa mara ya
kwanza, mwaka 2002, wakati kila anapozuru Ulaya, Amrouche amekuwa mwenyeji wake
na hasa nchini Belgium.
“Hawa wamekuwa kama ndugu na leo
wameamua kufika Championi na kuona tunavyofanya kazi zetu. Wanavutiwa na ubora
wa kazi zetu, leo wameona ni vizuri kufika hapa, basi tumefurahishwa kutokana
na ugeni wa makocha hawa mahiri na maarufu katika ukanda wetu,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment