Coastal Union ambayo imemaliza Ligi Kuu Bara kwa kipigo cha
bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar, wanachama wake wametoa kali.
Wanachama ambao wanaishi mkoani Tanga
walitoa ujumbe kwa uongozi wao wakionyesha kupinga mambo kadhaa yanayoonekana
kutokwenda sawa.
Lakini kilichoonyesha kweli mambo hayo
hayako vizuri ni wachezaji kwenda kuwaunga mkono wanachama hao mara baada ya
mechi hiyo kwisha.
Licha ya kuwa wamefungwa, lakini Coastal
Union walikwenda kuwapongeza wanachama wao kwa kuwaunga mkono na ujumbe mzuri
kwa viongozi.
Uongozi wa Coastal Union, umekuwa
ukishutumiwa kukataa kutoa kadi mpya za wachama, huku Kassim El Siagi ambaye ni
katibu mkuu akielezwa kuwa chanzo.
Siagi amekuwa akisisitiza kwamba lazima
kabla ya kuwakubali wanachama wapya, basi wawahakiki kwanza kwa kuwajadili.
Lakini katiba ya Coastal Union haina
kipengele hicho, hali inayoashiria ni uoga wa Siagi na wenzake wanaoohofia
huenda wanachama wapya watatokea watu wakaojitokeza kuwania nafasi zao.
0 COMMENTS:
Post a Comment