Kila mbabe ana mbabe wake, hilo ndilo
limetokea usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa PTA jijini Dar wakati bondia,
Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ alipopata kkibaya.
Bondia Sukkasem Kietyongyuth wa Thailand,
amempiga Miyeyusho kwa KO katika raundi ya kwanza, dakika ya kwanza sekunde ya
54.
Miyeyusho ambaye alianguka kama mzigo na
kuwashangaza mashabiki wengi, alionekana kushangazwa na kasi ya Mthai huyo.
Wakati anaingia ulingoni alionyesha
kujiamini, lakini baada ya dakika ya kwanza tu alikuwa ameishaanguka chini,
akajitahidi akainuka.
Lakini Sukkasem akaendeleza mashambulizi
mfululizo na kumuangusha tena, safari hii mwamuzi Emmanuel Mlundwa akalazimika
kumaliza pambano.
0 COMMENTS:
Post a Comment