April 8, 2014



Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema ana imani kubwa Azam FC watakuwa mabingwa wa Tanzania Bara.
Logarusic amesema Azam FC watakuwa mabingwa kwa kuwa watazipata pointi sita wanazohitaji kuwa mabingwa huku akisema wakishindwa, Simba ndiyo itaitibulia Yanga kuwa bingwa.

“Azam ndiyo watakuwa mabingwa, wana kikosi kizuri na kinaweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu. Najua watashinda mechi mbili.
“Lakini wakishindwa, basi sisi tutawatibulia Yanga. Najua tukikutana nao, basi hawataweza kutoka. Kama tukiwafunga Yanga, ubingwa utakwenda Azam FC,” alisema.
“Safari hii Yanga wajiimarishe kwa ajili ya nafasi ya pili na si kulazimisha ubingwa. Uhakika wa wao kupoteza pointi tukikutana nao, upo.

“Hivyo si lahisi kuwafikia Azam ambao wamejipanga mapema,” alisema Logarusic ambaye hii ni mara ya pili anazungumzia kuhusiana na Azam FC kuwa bingwa.

1 COMMENTS:

  1. Mjinga tu. Kwanini azungumzii timu yake anatafuta umaarufu kupitia yanga.yy ni mtaalamu afunge domo lake alioahidi wakati anaingia simba kashindwa kuyatekeleza sasa kawa mtabiri ajue salama ya azam na simba ni azam kushinda mechi zake akipoteza tu.kiama kwa simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic