MBEYA CITY COUNCIL FOOTBALL CLUB
TAARIFA KWA UMMA
UPOTOSHAJI UNAOTOLEWA DHIDI YA TIMU YETU KUELEKEA
MCHEZO WA TAREHE 13/4/2014
Kwanza nachukua
nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo wa mpira wa miguu na
wapenzi wa Mbeya City Fc popote pale walipo kwa kuiunga mkono timu yao muda
wote wa michezo ya ligi kuu inayoelekea ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini
nafasi ya wapenzi na washabiki katika kujenga timu imara na yenye ushindani
kama walivyofanya kwa timu yetu.
Timu yetu
ilianza ligi msimu huu 2013/2014 ikiwa na malengo ya kuchukua ubingwa au kuwa
katika nafasi za juu za ligi yetu.Hiyo ndiyo dhamila iliyokuwepo kwa
viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Michezo
miwili imesalia kwa timu yetu kabla ligi kuu ya Vodacom kumalizika katika msimu
huu 2013/2014.katika safari yetu ya ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu,
changamoto nyingi za kiutawala na za kimtazamo kutoka kwa wadau wote
wanaohusika na mchezo wa mpira wa miguu nchini tumezishuhudia .Changamoto hizo
ni ikiwemo upangaji wa ratiba usiyokuwa na uwiano mzuri,baadhi ya mechi
kuamuliwa vibaya na waamuzi wa mchezo,wizi wa mapato ya milangoni unaotokana na
mfumo mbaya wa uuzaji wa tiketi,uadilifu mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye
dhamana ya kusimamia mpira katika ngazi zote n,k.
Kuelekea
mchezo wetu wa tarehe 13/04/2014 dhidi ya AZAM FC kumezuka propaganda chafu na
ambazo si sahihi katika ukuzaji wa mpira hasa wa ligi ndogo kama ya Tanzania.
Nachukua nafasi hii kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo ambayo yamekuwa sehemu
ya propaganda hizo:
1.
Klabu imehaidiwa kununuliwa basi na hivyo inajiandaa
kutoa ushindi kwa kwa timu ya AZAM Fc na kuwarahisishia mazingira ya Ubingwa.
Halmashauri
ya jiji la Mbeya limekuwa katika mchakato wa kutafuta na kununua basi kwa ajili
ya matumizi mbalimbali ya Halmashauri ikiwemo
kutumiwa na timu zake ( Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo ligi kuu ya
michezo husika kwa kufuata sheria ya manunuzi ya Umma. Mchakato huo ulianza
tarehe 8/8/2013 halmashauri
ilipotangaza nia hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe hiyo kwa
tender no.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01
hii ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo
yake ya ndani kwa mwaka wa fedha
2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
Tangazo
hilo halikupata mzabuni mwenye sifa za kufanya usambazaji wa basi hilo hivyo
tangazo hilo lilirudiwa tena tarehe 12/2/2014 katika gazeti la majira kwa
Tender No. LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 (Re-advitised), Mchakato na
maandalizi ya ufunguaji wa ufanyaji wa
tathmini wa zabuni hiyo unaendelea kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma.
Pamoja na
mchakato huo hapo juu,pia klabu inaendelea na mazungumzo na wadau mbalimbali
wenye nia ya kuwekeza kwa udhamini wa bidhaa zao,moja ya maeneo ya udhamini ni
pamoja na ununuzi wa basi la wachezaji
taratibu na makubaliano haya yatakapo kamili umma wa wapenda mchezo wa
mpira wa mguu utajulishwa.
Hivyo
propaganda hiyo kuwa klabu imehongwa basi si za kweli na si sahii ila zina nia
ya kuidhalilisha timu yetu.
2.
Propaganda kuwa Mwalimu Juma Mwambusi kanunuliwa
nyumba Maeneo ya chamazi ili apange kikosi dhaifu siku ya mchezo tarehe
13/4/2014.
Mwalimu(Kocha)
Juma Mwambusi ni muajiliwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya,kwa maana hiyo ni
mtumishi wa Umma. Mwalimu Mwambusi amekuwa na timu yetu kwa muda mrefu sasa na
ataendelea kuwepo.Kumekuwepo na maneno yasiyofaa dhidi ya mwalimu wetu toka
mzunguko wa pili wa ligi kuanza,maneno haya yamekuwa na nia ya kuaribu muenendo
wa timu ili ianze kufanya vibaya lakini zaidi ya hapa yana nia ya kumdhalilisha
mwalimu wetu na taaluma ya ukocha nchini.
Mwalimu
amefedheheshwa sana na taarifa hizo.
3.
Propaganda kuwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza
wamepewa hongo wacheze chini ya kiwango 13/4/2014.
Wachezaji
ndiyo wachezaji wenye nidhamu kubwa katika ligi ya mwaka huu ndani na nje ya
uwanja muda wote,ni waadirifu na wanajua wanataka nini.Mpira ndiyo ajira yao
kama watumishi wa umma ndani ya Halmashauri ya jiji la Mbeya.Hawajawahi na wala
hawatawahi kuchukua rushwa kwa lengo la kupanga matokeo.
Klabu yetu
haisadiki katika upangaji wa matokeo ya mchezo wa mpira wa miguu kwani tunajua
fika kuwa hakutaisadia kama klabu lakini pia kama taifa katika kuendeleza mpira
wa miguu nchini.
Hitimisho,
Mchezo wa
mpira wa miguu una matokeo matatu kushinda,kushindwa na kutoka sare. Klabu
inaamini kuwa timu iliyojiandaa vizuri kama yetu inastahili kupata matokeo
mazuri uwanjani.Falsafa mojawapo ya timu yetu ni kushinda mechi kwa kucheza
mpira unaovutia na kuwaburudisha watazamaji.
Tuhuma
mbalimbali za upangaji matokeo katika ligi yetu zimeanza kuota mizizi hasa ligi
inapoingia mzunguko wa pili ,katika suala hili kama ambavyo linataka kuhusishwa
nasi yawezekana propaganda hizi kwa upande wa timu inayotuhumiwa kuandaa
michakato hiyo wana uzoefu nalo na yumkini ndiyo chachu ya mafanikio yao mpaka
kufikia hatua hiyo waliofikia sasa.
Kama timu
hiyo inauwezo wa kirasilimali wa kufanya uovu huo wote iweje ishindwe kuwa na
timu imara na ya ushindaji mpaka itegemee kutafuta wachezaji wa timu pinzani
kupata matokeo mazuri?
Timu yetu
ndiyo timu pekee changa miongoni mwa timu tano zinazoongoza msimamo wa ligi
yetu kwa sasa,si hivyo tu bali ndiyo timu pekee inayoundwa na wachezaji wengi
wapya katika ulimwegu wa soka na inayoundwa na Watanzania watupu kuanzia
wachezaji,benchi la ufundi pamoja na viongozi.Hii inathibisha kuwa kama taifa
tunaweza kufanya kazi nzuri bila kutegemea wachezaji toka nje baadhi yao
wasiokuwa na tija.
Mpira ni
ajira hatuna budi kuuratibu vema ili kutoa nafasi inayostahili kwa vijana wetu
ili kupunguza tatizola ajira nchini lakini pia kutumia vipaji vyao kulipa taifa
muonekano stahili.
Mamlaka
zinazohusika hazina budi kuanza kufuatilia na kuchukua hatua kali kwa baadhi ya
timu zinzohusishwa na upangaji wa matokeo ili kulinda heshima ya mchezo huo
bila kuogopa uwezo wa rasilimali wa timu hizo.
E.E.Kimbe
KATIBU
MKUU
MCC
FC
9.04.2014
0 COMMENTS:
Post a Comment