MSHAMBULIAJI kinda wa Klabu ya Borussia Dortmund, Youssoufa Muokoko usiku wa kuamkia leo amefunga bao la kwanza ndani ya Ligi ya Uingereza maarufu kama Bundesliga na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kufunga kwenye ligi hiyo.
Nyota huyo mwenye miaka 16 amevunja rekodi ya nyota wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz ambaye alifunga akiwa na miaka 17 ilikuwa dhidi ya Bayern Munich akiwa Mei 2020.
Dortmund ambayo ilimchimbisha kocha wao Lucien Favre wiki iliyopita baada ya kupokea kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya VfB Stuttgard nafasi iliyochukuliwa na Edin Terzic ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya Union Berlin na Moukoko alifunga bao lake la kwanza.
Nyota huyo mzaliwa wa Cameroon amesema kuwa ni furaha kubwa kwake kufunga kwenye mchezo huo ilikuwa dakika ya 60 licha ya timu yake kupoteza jambo ambalo litawafanya wapambane kwa ajili ya mechi zao zijazo.
Mabao ya wapinzani wao yalipachikwa na Taiwo Awonyi dakika ya 57 na lile la ushindi lilipachikwa dakika ya 78 na Marvin Friedrich alipachika bao la ushindi na kuifanya Union Berlin kusepa na pointi tatu mazima Uwanja wa Alle Forsterel.
Matokeo hayo yanaifanya Dortmund iwe nafasi ya nne na pointi 22 baada ya kucheza mechi 13 Bayer Leverkusen ni vinara wakiwa na pointi 28.
Ligi ya Uingereza, Bundeliga!!!
ReplyDeleteMwandishi umechukia andika Tena habari hii
ReplyDeleteHivi blog hii ina waandishi au waandikaji??
ReplyDeleteMmmmmmh
ReplyDeleteSalehjembe chukua hatua. Blogu yako inapoteza heshima na weledi wake kila siku. Leo ndio mwisho mimi kuisoma. Enough is enough.
ReplyDelete