Wakati Simba imeshaanza harakati za kumnasa Amissi Cedric ili
ajiunge nayo msimu ujao, kuna taarifa timu za Ubelgiji na Ulaya Mashariki
zimeanza mipango ya kumnasa.
Cedric, raia wa Burundi, anayekipiga katika kikosi cha Rayon
Sports ya Rwanda, amekuwa kivutio kwa Simba tangu msimu uliopita na siku chache
zilizopita ilifanya naye mazungumzo baada ya kuja nchi akiwa na timu yake ya
taifa ya Burundi ambayo ilishinda kwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki jijini
Dar.
Kocha Mkuu wa Kenya, Harambee Stars, Adel Amrouche,
amelithibitishia Championi Jumatano kuwa, Cedric sasa ni lulu nchini Ubelgiji
anakotokea.
“Ni kweli kuna zaidi ya timu mbili za daraja la pili na daraja la
kwanza ambazo zinamtaka Amissi, hata jana nimezungumza naye,” alisema Amrouche
ambaye aliwahi kumfundisha mshambuliaji huyo wakati akiwa Kocha Mkuu wa Burundi
kabla ya kutua Harambee Stars.
“Lakini kuna timu moja kutoka Ulaya Mashariki pia imeonyesha nia
ya kutaka kumchukua, sasa sijui kama Simba itawahi au vipi.”
Ukiachana na Amrouche, Kocha Mkuu wa Rayon Sports, Luc Eymael raia wa Ubelgiji ameliambia gazeti
hili, tayari mchezaji huyo ana mwaliko mmoja wa kufanya majaribio Ubelgiji
anakotokea.
“Nafikiri anaweza kwenda Ubelgiji kufanya majaribio kwenye klabu
ya daraja la pili, viongozi waliniambia kuhusiana na hilo lakini sina uhakika
itakuwa ni lini. Ligi imebakiza mechi moja kwisha, hivyo anakuwa huru kwenda,”
alisema.
Cedric ndiye mfungaji bora wa Rwanda msimu uliopita baada ya
kutupia nyavuni mabao 16, lakini pia anaongoza msimu huu akiwa na mabao 13 huku
akiwa na nafasi kubwa ya kuitwaa nafasi hiyo kwa mara nyingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment