April 30, 2014

NONGA (WA KWANZA KULIA)AKIWA NA KIKOSI CHA MBEYA CITY.

Mshabuliaji wa Mbeya City, Paul Nonga, amezikataa timu za Simba na Yanga kwa kusema kuwa hafikirii kuondoka katika timu hiyo.


Nonga ameonyesha kiwango cha hali ya juu akiwa na timu hiyo ya mkoani Mbeya ambayo imemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu na amesema anataka kuendelea kukaa kwenye timu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Nonga alifunguka kuwa, hafikirii kuondoka Mbeya City kwa kuwa mtazamo wake ni kuhakikisha anaisaidia timu hiyo ili iweze kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu ujao.
“Kwa kweli sifikirii kuondoka Mbeya City  kwani ndiyo timu iliyoniibua na nitabaki hapahapa kwani ushindani tulioutoa kwenye ligi iliyoisha unatokana na mshikamano tuliokuwa tukiuonyesha.

“Tunavyoishi katika kambi ya Mbeya City ni kama ndugu. Hakuna tatizo lolote kwani tumezoea mazingira hayo ikiwa ni pamoja na uongozi kutupa ushirikiano wa kutosha.
“Unadhani wote tukijazana Simba na Yanga nani ataijenga Mbeya City?  Kwani inaweza kubomoka msimu ujao iwapo wachezaji wengi wataondoka na kuifanya timu ishuke kiwango, lengo letu ni kutwaa ubingwa msimu ujao tukiwa na Mbeya City.

“Kiujumla ligi ilikuwa ngumu kwa kuwa kila timu tuliyokuwa tukikutana nayo ilikuwa inatukamia na kutufanya tupoteze rekodi yetu ya mzunguko wa kwanza ya kutofungwa, tulifanya makosa na wenzetu wakayatumia, katika mzunguko wa kwanza walikuwa hawatujui,” alisema Nonga.
SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic