April 7, 2014


Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngongoro Heroes) inarejea nchini leo (Aprili 7 mwaka huu) kutoka Kenya ambapo jana (Aprili 6 mwaka huu) ilicheza mechi ya michuano ya Afrika.


Ngorongoro Heroes inayonolewa na John Simkoko itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.25 mchana kwa ndege ya Kenya Airways ilitoka suluhu na wenyeji Kenya katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kanyetta uliopo mji wa Machakos.


Timu hizo zitarudiana jijini Dar es Salaam wiki tatu baadaye ambapo itakayofuzu itacheza raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini. Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 zitachezwa mwakani nchini Senegal.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic