Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) limekubaliana na uamuzi uliofanywa na Kamati ya Maadili katika malalamiko
mawili ambayo iliyawasilisha mbele yake, hivyo haitakata rufani.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine aliwasilisha
mashauri mawili mbele ya Kamati hiyo iliyoongozwa na William Erio. Malalamiko
ya kwanza yalikuwa dhidi ya waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA), Oden Mbaga na Samwel Mpenzu na
wakufunzi wa waamuzi Riziki Majala na Mchungaji Army Sentimea.
Wote aliwalalamikia kwa kuwafanyisha
mitihani (wakufunzi), na waamuzi kufanya mitihani hiyo kinyume na utaratibu
pamoja na kughushi matokeo.
Kamati katika uamuzi wake iliiagiza
waamuzi hao kufanya upya mtihani huo katika robo inayofuata ambapo wakifaulu
waendelee kuchezesha mechi. Waamuzi wa FIFA hufanya mitihani hiyo mara nne kwa
mwaka.
Kwa upande wa shauri dhidi ya Ofisa
Takwimu wa TFF, Sabri Mtulla ambaye alilalamikiwa kwa kuidanganya Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi dhidi ya mchezaji
Emmanuel Okwi, Kamati iliagiza suala hilo liwasilishwe upya pamoja na ushahidi
wa kuthibitisha malalamiko hayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment