KILA zama zina mfalme wake, hiki ndiyo kipindi ambacho karibu kila mtu
anayevutia na kocha kijana anayeonyesha uwezo mkubwa analazimika ku muangalia Diego Pablo Simeone.
Hakuna ubishi ndiye kocha bora na mwenye uwezo wa juu katika wale
wanaochipukia katika kipindi hiki kutokana na mafanikio makubwa yanaonekana
akiwa na Altetico Madrid.
Tokea aanze kuifundisha timu hiyo mwaka 2011, amekuwa na mafanikio
makubwa sana kwa kuwa ameiwezesha kubeba makombe matatu makubwa na maarufu
duniani kote, moja likiwa ni lile la Copa de Rey lakini kabla alichukua mawili
ya kimataifa ya Europa na Uefa Super Cup.
Hicho kinaweza kuwa ndiyo kigezo cha kwanza ambacho ni uwezo wa kubeba
zawadi lakini kigezo cha sasa ni kufanikiwa kufika Ligi ya Mabingwa kwa
kishindo akiwapindua makocha na timu bora tena si kwa kubahatisha.
Robo fainali aliibwaga Barcelona yenye nyota kibao, ikaonekana huenda kwa
kuwa ni timu ya Hispania wameizoea, kaonyesha sivyo kwani nusu fainali na
Chelsea, mechi ya kwanza jijini Madrid ikawa suluhu, waliporudiana London,
akampa Jose Mourinho kichapo cha mabao 3-1 na kuifuata Real Madrid fainali.
Sasa Atletico Madrid inapewa nafasi ya kubeba kombe kwa kuwa inakutana na
Real Madrid, si timu ya kuihofia sana badala yake watapambana nayo kama
mpinzani, mtani na hasimu.
Ile sifa ya kocha kijana, mwenye uwezo mkubwa na mipango ya kutosha
aliyokuwa nayo Mourinho, hakuna ubishi imehamia kwa Simeone. Lakini itakamilika
kama atatwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Lisbon, Ureno, Mei 21.
Kuna mambo wanafanana kama vile
kufundisha katika nchi zaidi ya moja baada ya kutoka kwao, Mourinho baada ya
Ureno amekwenda England, Italia na Hispania na Simeone alipoondoka kwao
Argentina amefundisha nchini Italia na Hispania. Pia wamekuwa hawakai na timu
muda mrefu kama Alex Ferguson na Arsene Wenger.
Lakini Simeone ana kitu cha ziada kwa kuwa amecheza soka katika ‘levo’ za
juu. Pia amewahi kuchukua ubingwa wa La Liga pia Copa del Rey akiwa na Atletico
Madrid kama mchezaji, amechukua makombe kadhaa akiwa kwao Argentina na Italia
‘Serie A’. Pia amecheza Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa ya
Argentina.
Kwa ujumla amechukua makombe 12 yanayotambulika akicheza soka katika ligi
za nchi za Argentina, Italia na Hispania, wakati Mourinho hajawahi kubeba kombe
hata moja akiwa mchezaji.
TAKWIMU:
Akiwa
mchezaji:
NCHINI MECHI MABAO
Argentina 113 17
Italia 202
32
Hispania 198 35
JUMLA 513 84
Akiwa
kocha:
Timu
alizofundisha:
Racing 2006-06
Estudiantes 2006-07
River Plate 2007-08
San Lorenzo 2009-10
Catania 2011-11
MECHI SHINDA
SARE POTEZA WASTANI
348 19
72 86 54.60%









0 COMMENTS:
Post a Comment