Lionel Messi amekuwa
mwanasoka anayelipwa zaidi kuliko wengine wote kutokana na ofa aliyopewa kwenye
mkataba wake mpya na Barcelona.
Mwanasoka huyo nyota
kutoka Argentina, atakuwa akipata euro milioni 20 kwa msimu baada ya makato ya
kodi, lakini kuna nyongeza ya milioni 3 ambayo itaendana na amefanikiwa vipi
kwa msimu.
Kutokana na malipo hayo,
Messi atakuwa amempiga bao mpinzani wake mkubwa Cristiano Ronaldo, anayelipwa
euro milioni 18 kwa msimu baada ya makato ya kodi.
Namba tatu sasa anakuwa
Zlatan Ibrahimovic wa PSG ya Ufaransa ambaye baada ya kodi kwa msimu, analamba
euro milioni 14.67.
Namba nne inakwenda kwa Falcao,
mshambuliaji wa zamani wa Atletico Madrid ambaye sasa anakipiga Monaco ya
Ufaransa ambaye baada ya makato ya kodi anachukua euro milioni 14.5 kwa msimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment