Beki wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua ‘Mr Pisha Njia’ ametangazwa
kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo wa msimu uliopita na kufanikiwa kuwabwaga
wachezaji wote katika kikosi cha timu hiyo.
Joshua ambaye kipindi cha nyuma hakuwa na nafasi ya kudumu katika
kikosi cha timu hiyo, juzi Alhamisi alitangazwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu
hiyo, Hans van Der Pluijm kuwa ndiye mchezaji bora wa msimu uliopita wa klabu
hiyo.
Pluijm amesema kuwa amempatia tuzo hiyo Joshua kutokana na kuifanya
kazi yake kwa ufanisi mkubwa kwa kuzingatia maagizo aliyokuwa akimpatia.
“Mchezaji bora wa msimu uliopita katika kikosi changu ni Oscar
Joshua, kwa sababu amekuwa akizingatia kila kitu nilichokuwa nikimwelekeza
uwanjani na nje ya uwanja.
“Siyo kwamba ana uwezo mkubwa sana wa kucheza soka lakini uwezo wake
wa kuzingatia yale yote niliyokuwa nikimtaka kuyafanya uwanjani na nje ya
uwanja ndiyo kigezo kikubwa kilichonifanya nimpatia tuzo hiyo,” alisema Pluijm.
Kabla ya Pluijm kuchukua mikoba ya kuifundisha Yanga, Joshua alikuwa
katika wakati mgumu na kuna wakati alikuwa anataka kuondoka klabuni hapo
kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Aliyekuwa
kocha mkuu wa hiyo kwa wakati huo Ernie Brants alikuwa akimhusudu, David
Luhende lakini baada ya kuondoka na kuja kwa Pluijm, Joshua aliweza kung’aa na
kupata nafasi ya katika kikosi cha kwanza cha Yanga na hatimaye sasa ni mmoja
kati wa wachezaji wanaounda timu ya taifa, Taifa Stars.
0 COMMENTS:
Post a Comment