Kamati ya uchaguzi ya Simba imeendelea kupambana ili kumaliza
mapingamizi kabla ya kuyatolea uamuzi.
Kamati hiyo chini ya mwanasheria maarufu nchini, Dokta Damas
Daniel Ndumbaro ilianza kazi jana, lakini leo imeendelea siku nzima kuchambua
utetezi uliofanywa jana pamoja na kuwahoji walioweka mapingamizi.
Hata hivyo, pamoja na kuwa na taarifa kuwa uamuzi wa mapingamizi
hayo ungetangazwa leo, mambo yamekuwa tofauti.
Kama kamati hiyo itakuwa imemaliza kazi, imeelezwa mabosi wa
kamati hiyo wataweka mambo hadharani hadharani kesho.
Imeelezwa ugumu huo wa kamati kufanya kwa kazi siku mbili
mfululizo ni kutokana na wingi wa mapingamizi hayo.
Wagombea wa urais, Evans Aveva na Michael Wambura wamewekewa
mapingamizi, lakini wale wa makamu rais.
Baada ya majibu ya mapingamizi hayo, waliokatwa watapewa nafasi
ya kukata rufaa kwenye kamati ya rufaa chini ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF).
Uchaguzi mkuu wa Simba umepangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment