Kiungo wa zamani wa Arsenal,
Patrick
Vieira ametembelea jijini Dakar, Senegal kusaidia watoto kupata elimu na kupewa
nafasi ya kushiriki michezo nafasi yake ikidhaminiwa na Western Union.
Kiungo huyo nyota wa zamani wa Arsenal alikuwa mjini humo jana na leo alitarajiwa kurejea Ulaya kuendelea na shughuli zake.
Kiungo huyo nyota wa zamani wa Arsenal alikuwa mjini humo jana na leo alitarajiwa kurejea Ulaya kuendelea na shughuli zake.
Vieira ambaye ni Mfaransa mwenye asili ya
Senegal, pia sasa ni mhusika katika kukuza vipaji katika klabu ya Man City
ambao ni mabingwa wa England, alipata nafasi ya kucheza na watoto, pia
kuzungumza nao na kutoa mafunzo.
Pia safari yake hiyo kwa maendeleo ya
vijana iliungwa mkono na Unicef na alionekana kuwa mwenye furaha kurejea katika
nchi aliyokulia kabla ya kuhamia Ufaransa.
0 COMMENTS:
Post a Comment