Uongozi wa Yanga umesema ulijaribu kila linalowezekana kumzuia kiungo wao Frank Domayo.
Mmoja wa viongozi wanaohusika na usajili amesema walianza kumpa mkataba kiungo uyo miezi minne iliyopita.
“Lakini alikuwa anasema tumsubiri mjomba wake kwanza wajadiliane. Tulifanya hivyo zaidi ya mara tatu lakini alikataa,” alisema.
Lakini msemaji wa Yanga, Baraka Kizugutio akasisitiza kuwa kweli walimpa Domayo mkataba akasema..
“Mara ya kwanza alisema tumsubiri mjomba wake, huyo ndiye wakala wake na jana tumesikia ndiye aliyempeleka Azam. Sasa tungefanya nini zaidi ya hapo.
“Yanga imekuwa na wachezaji wengi wakaondoka na ikaendelea kuwepo, mwache aende,” alisema Kizuguto.
Usajili wa Domayo kwenda Azam FC umekuwa gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka nchini huku wale wa Yanga wakiulaumu uongozi wao kulala na kutoa ruhusa kwa Azam FC kumnasa Didier Kavumbagu na baadaye Domayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment