Mashabiki wa Yanga wamevamia nyumbani kwa kiongozi wa zamani wa timu hiyo na kuomba msaada.
Mashabiki hao wamevamia nyumbani kwa Davis Mosha jijini Dar es Salaam na kumtaka kuingia suala la usajili kwa kuwa Azam FC imeshabeba wachezaji wawili, Didier Kavumbagu na Frank Domayo.
Akizungumza wakati akihojiwa redioni, Mosha alisema mashabiki hao wamemuomba aingie na kuikoa Yanga.
“Kweli wamevamia nyumbani kwangu na kunitaka nisaidie kuokoa wachezaji wasichukuliwe tu.
“Lakini wakashauri nigombee uchaguzi unaofuata, nimewasikiliza. Lakini siwezi kusema lolote kwa kuwa mimi siongozi sasa.
“Ila hao viongozi wa Yanga wanapaswa kujua kuwa hata kama wako ambao hawatagombea, wasiiache tu Yanga iende hivihivi, kama kuna jambo la kufanya wafanye kuikoa,” alisema.
Mosha aliwahi kuwa makamu mwenyekiti kabla ya kuamua kuachia ngazi.
http://www.bbc.com/sport/0/football/27235859
ReplyDelete