Nyota wa
zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila amewaonya wanaoanzisha malumbano na
Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kuwa makini wasisababishe vurugu.
Lunyamila
amewataka watu wanaopinga Manji kuongezewa muda wa mwaka mmoja kuwa wazalendo
kwa Yanga.
MANJI |
Lunyamila amesema uamuzi wa kumuongezea Manji mwaka mmoja
ni wa busara na wanachama waliliona hilo.
madaraka.
“Wanachama
4,000 waliokuwa kwenye mkutano wamefikia uamuzi ule, nani atahoji uhalali wa
kufanya hivyo," alisema Lunyamila.
"Yanga
sasa iko kwenye suala la usajili na kutafuta kocha, wasituvuruge, wawe wazaendo
na ndiyo maana walitakiwa kuwepo kwenye kikao.
LUNYAMILA |
"Kama
ilishindikana, basi wanatakiwa kukubali uamuzi wa wengi kwa kuwa waliofanya
vile ni watu wenye akili timamu," alisema Lunyamila.
"Angalia
alikuwepo hadi Mama Karume ambaye ni mzoefu na mdhamini wa Yanga, sasa vipi
ionekane ni tatizo.
"Au
wanataka kuichanganya Yanga katika kipindi hiki cha usajili? angalia Simba
walivyo katika hali mbaya kutokana na malumbano ya uchaguzi, haijulikani nani
atafanya usajili au anasimia mambo ya klabu," alisema Lunyamila.
Wanachama
wachache wamekuwa wakipinga Manji na uongozi wake kuongezewa mwaka mmoja.
Manji alipewa nyongeza ya miaka nane na
wanachama hao, lakini akasisitiza hataweza na kuomba angalau mwaka mmoja
uchaguzi usogezwe mbele, wanachama waliokuwa kwenye mkutano huo wakakubali kwa
umoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment