Uchaguzi mkuu wa viongozi wa
klabu ya Simba umeanza rasmi sasa hivi.
Tayari wanachama hao
wameanza kupiga kura kuchagua viongozi wao wapya watakaoiongoza Simba kwa miaka
minne ijayo.
Nafasi tatu za rais, makamu
wa rais, wajumbe wa kamati ya utendaji moja ikiwa ni maalum kwa kinamama, ndiyo
zinazogombewa leo.
Mgombea Evans Aveva anapewa
nafasi ya kuwa rais mpya wa Simba, lakini Andrew Tupa pia anaweza kutoa
upinzani, si wa kumdharau.
Upinzani mkali unaonekana
upo kwenye nafasi ya makamu wa rais inayowaniwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’,
Swed Nkwabi na Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
0 COMMENTS:
Post a Comment