June 29, 2014




Mwanamama Jasmin Badar anayegombea nafasi ya kamati ya utendaji ya klabu ya Simba kwa upande wa wanawake amewavutia wanachama wengi kutokana na kujieleza kiufasaha.
Katika uchaguzi wa Simba unaendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, Jasmini alionyesha uwezo mkubwa wa kujieleza.
Jasmini aliwashangaza wengi ukumbini hapo kutokana na maelezo yake kuwa yamenyooka.

Mwanamama huyo sasa ni mke wa beki wa zamani wa Simba, Victor Costa Nampoka.
Lakini bado uchaguzi ni mgumu na uamuzi wa nani achukua nafasi hiyo uko mikononi mwa wanachama hao wa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic