Wakati Xabi Alonso alipotua
Bayern Munich, wengi walilalamika kwamba hakukuwa na haja ya timu hiyo
kumchukua mkongwe huyo kuziba pendo la Toni Kroos aliyekwenda Real Madrid.
Badala yake wakasisitiza
wangeweza kuwapa nafasi vijana.
Lakini kadiri siku
zinavyosonga mbele, Xabi Alonso amezidi kutoa somo kwa kufanikiwa kuwa mchezaji
bora wa mechi mara mbili katika mechi tano.
Kama hiyo haitoshi, Alonso
amefanikiwa kugusa mpira mara 679, huku akipiga pasi 558 zilizofika ukiwa ni
wastani wa 89% ambao ni wa juu
kabisa.
Katika mechi wakati Bayern
ilipoivaa Cologne jana, Alonso alipiga pasi 175, si mchezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment